About us

Showing posts with label Sports. Show all posts
Showing posts with label Sports. Show all posts

Tuesday, January 12, 2016


Aliye kuwa raisi wa shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatterna Mwanasheria wake anatarajiwa kuwasilisha rufaa ya mteja wake ya kupinga kufungiwa miaka minane kujishughulisha na masuala ya soka.

Hata hivyo kamati ya nidhamu ya FIFA imewasilisha sababu za kuchukuliwa kwa hatua za nidhamu dhidi ya viongozi hao waandamizi wa zamani wa soka Blatter na mwenzake, Michel Platini. Mwezi Disemba aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini walifungia kwa kipindi cha miaka minane baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja kanuni na sharia za FIFA. Kwa upande wake pia mwanasheria wa Platini anasema kuwa anatarajia kukata rufaa kwa kupinga maamuzi ya FIFA.
Continue reading

Friday, December 11, 2015

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye
Jana Rais John Pombe Magufuli alitangaza baraza lake la mawaziri baada ya watu kusubiri kwa muda mrefu kusikia ni akina nani watapewa majukumu ya kusimamia wiara mbalimbali kwenye serikali ya wamu ya tano ambayo imeanza kwa kasi ya aina yake.
Kwenye upande wa michezo, Dr. Magufuli amemteuwa Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utaduni, Wasanii na Michezo. Wanamichezo wengi wanahitaji kuona Tanzania inafanya mabadiliko makubwa kaika nyanja ya michezo mbalimbali.
Swali linakuja, je Waziri Nape Nnauye atafanikiwa kuleta mabadiliko kwenye nyanja ya michezo akiwa ni kiungo kati ya serikali na viongozi wa vyama vya michezo hapa nchini ambapo kwa miaka kadhaa Tanzania imekuwa haifanyi vizuri katika mashindano ya kimataifa kwenye michezo husika?
Mchambuzi wa masuala ya michezo wa kituo cha Clouds Media Group Shaffih Dauda jana alisikika kupitia kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM akitaja matarajio yake kutoka kwa Waazriri huyo mpya aliyepewa majukumu ya kusimamia Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.
Dauda amesema yeye anategemea Nnauye atafanya utafiti kwa kushirikiana na wadau wa michezo ili kubaini changamoto zilizopo, kujua wapi pa kuanzia kuzitatua changamoto hizo zinazoikabili sekta ya michezo kwa muda mrefu.
“Kikubwa ambacho mimi nakitegemea kutoka kwake (Nape Nnauye) ni kutafuta wadau na kukutana nao kujua changamoto, kujua wapi pa kuingilia na kutokea halafu baadae akisha maliza hayo, ni kukubali kukaa katikati ya serikali na sekta ya michezo. Kama tulivyosikia kauli ya Rais akisisitiza ‘kutumbua majipu’ na huku kuna majipu mengi sana ambayo yanahitaji kutumbuliwa”, alisema Dauda wakati akitoa maoni yake juu ya kuteuliwa kwa Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.
“Kwahiyo yeye pia angaalie katika jicho hilo kwsababu hawezi kufanya kitu kama bado wale ambao wameingia ‘kimagumashi’ wataendelea na ataruhusu waendelee kuwepo au ataruhusu watu ambao hawana mchango waendelee kuingia kwenye sekta ya michezo”.
“Na hiyo inategemea na namna ambavyo yeye atakuwa anaichukulia sekta ya michezo, kama atakuwa anaona ni ya kawaida tu basi tutaendelea kubaki hivyohivyo, lakini kama ataichukulia kwa uzito wake naamini pia majipu mengi huku yatatumbuka”.
Wadau wengi wa michezo nchini wanasubiri kwa hamu kujua mipango ya kuhakikisha michezo hapa nchini inakuwa na tija na inakuwa na maendeleo siyo tu kwa taifa lakini pia kwa wanamichezo husika.aa
Continue reading

News-Sacked
Kocha Louis Van Gaal wa Manchester United anaweza kutimka klabuni hapo mwisho wa msimu huu pamoja na kuwa bado ana mkataba hadi msimu ujao. Taarifa zilizoandikwa na magazeti mbalimbali nchini England zinasema hali sio shwari sana kwa future ya kocha Louis Van Gaal ambaye sasa presha ni kubwa sana kutokana na kutolewa kwa Manchester United klabu bingwa Ulaya sanjari na mwendo wa kobe katika ligi kuu soka nchini England.
Swali kubwa ni nani atakae rithi mikoba ya kocha huyu endapo ataondoka klabuni hapo? Alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa msaidizi mwaka 2013 mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Ryan Giggs, taa ya kijani ilianza kuwaka kwa mkongwe huyo aliyecheza kwa mafanikio sana chini ya kocha Sir Alex Ferguson.
Habari zinasema kuwa, Ryan Giggs ndiye chaguo la mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo Ed Woodward na kwamba ndiye atakaye kuwa mrithi wa Van Gaal endapo tu mholanzi huyo ataondoka Old Trafford.
Ryan Giggs amekaa na kocha Sir Alex Ferguson huku akishuhudia utawala wa Manchester United barani Ulaya na ligi za nyumbani lakini sasa amekua akiumia hali akiwa msaidizi tangu 2013. Kimya chake kinaweza kuwa cha kisiasa kuwatega United kuhusiana na kupewa nafasi ya ukocha mkuu baada ya Louis Van Gaal.
Lakini kocha wa Bayern Munich Pep Guadiola anaweza kuwa mrithi wa Van Gaal endapo tu Manchester United itaamua kutafuta mwalimu kutoka nje ya Uingereza. Tayari kuna taarifa za chinichini kuhusu nia ya Pep Guadiola kuwa na mahaba na United, huku hadi sasa akiwa hajasema chochote kuhusu mkataba wake.
Continue reading



Kwa mara ya kwanza jukwaa la Ballon D’or litapata ugeni mpya wakati mshambuliaji wa kibrazil Neymar Dos Santos atakapoungana na wafalme wawili wa tuzo hizo ambao wameitawala tuzo hiyo zaidi ya miaka 8 – Cristiano Ronaldo na Lionel Messi – itakapofika January 2016. Kama isingekuwa siasa za soka basi mbrazil huyo angeweza kushika nafasi ya pili nyuma Lionel Messi. Lakini hii ni ‘era’ mpya ya soka.
IMG_1225.JPGKatika miaka 8 iliyopita Ballon D’or imekuwa inatawalia na Messi dhidi ya Ronaldo, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda inaonekana mtu wa kupambana na Messi si Ronaldo tena ambaye umri unamtupa – anakaribia kutimiza miaka 31, Ni Neymar ambaye nyota yake inazidi kung’aa kila kukicha.
Pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana vizuri na washambuliaji wengine wa Barca, pia Neymar ameonyesha anaweza ku-control mechi kama ilivyo kwa Messi, tofauti na Ronaldo.
Wadau na wachambuzi wengi wa michezo duniani wanaamini katika kipindi kifupi kijacho Neymar atakuja kuwa mwanasoka bora zaidi duniani, mimi nikiwepo kwenye kundi hilo na hizi ndio sababu zangu.
  1. Kupafomu vyema Anapokosekana Messi 
281D9A4600000578-3060793-image-a-29_1430309883032Unapocheza pembeni ya Lionel Messi, vitu huenda kiurahisi zaidi. Wakati Messi alipoumia hivi karibuni kwa zaidi ya mwezi mmoja, wachambuzi wengi walikuwa na mashaka na uwezo wa Neymar kuziba pengo na kuisadia Barcelona kama ilivyokuwa kwa Messi. Lakini matokeo yake, Neymar akafanya vizuri zaidi katika kuisadia Barcelona kushinda kila mara na sasa wapo juu ya kilele cha msimamo wa ligi na wamefuzu raundi ya 16 bora wa UEFA Champions League. Kuziba pengo la mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kuugusa mpira sio jambo rahisi kabisa lakini kwa namna Neymar alivyohimili presha na kuifanya kazi, inaonyesha wazi dalili za world class player mwenye uwezekano wa kutwaa  Ballon d’Or hivi karibuni.
  1. Uwezo Binafsi
150606223921-neymar-champions-league-final-super-169Yes, ni kweli hivi sasa Neymar amekuwa mchezaji anayecheza kitimu zaidi kuliko ilivyokuwa zamani. Hata kuna wakati timu ikiwa inacheza vibaya, Neymar amekuwa akijitokeza na kuchukua majukumu ya timu kutumia uwezo binafsi kuiletea timu matokeo chanya. Anaweza kuchukua ‘vijiji’  kiurahisi na kuiletea madhara makubwa ngome ya timu pinzani, si rahisi kutabiri nini atafanya wakati mwingine. Ni mchezaji ambaye ni vigumu kumkaba na mbinu zake kali alizonazo miguuni na kadri anavyoendelea kucheza na kupata uzoefu, Neymar yupo njiani kuwa mwanasoka bora zaidi duniani.
3. Uwezo wa Kuwachezesha Wenzie
neymarhighs_sf6ly9x16vcg10w421p262n2m-1425743415Baadhi ya wachezaji  bora duniani wamekuwa bora kutokana na ukweli kwamba wana uwezo wa kuwachezsha wachezaji wenzao. Mchezo wa Neymar huko nyuma ulikuwa umeegemea katika uwezo wake binafsi zaidi na kuna muda alifanya iwe rahisi kwa wapinzani kuzuia dhidi ya timu yao. Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda amekuwa sehemu muhimu ya timu, Neymar ameuelewa zaidi mfumo na sasa anawachezsha mpaka wachezaji wenzie. Takwimu zinaonyesha hivi sasa anapiga sana pasi kuliko ilivyokuwa zamani, hili la kupiga pasi limeongeza kutokutabirika kwa mchezo wake na kuzidi kuwapa wakati mgumu wanaomzuia kumkaba. Hili limeleta mabadiliko makubwa katika staili ya uchezaji wa Neymar – pia limemletea mafanikio kuliko mwanzoni.
  1. Influence in the International side :
Neymar of Brazil celebrates his second goal against Turkey during their international friendly soccer match at Sukru Saracoglu stadium in Istanbul November 12, 2014. REUTERS/Murad Sezer (TURKEY  - Tags: SOCCER SPORT)Wanaompinga Neymar wana utetezi wao kwamba mchezaji huyo anafanya vizuri Barcelona kutokana na sapoti ya Messi na Suarez lakini kiwango cha Neymar kinapoangaliwa kwenye level ya timu ya taifa – ushahidi unaonyesha Neymar ndio msingi mkuu wa mashambulizi ya timu ya Selecao. Nahodha huyo wa Brazil ameitawala safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na ameiongoza kimafanikio mpaka sasa akiwa na miaka 23 tu. Bado ana safari ndefu kuendelea kuwa na kiwango kikubwa alichonacho. Ameyabeba majukumu ya unahodha vizuri sana na anaamini hivi karibuni ataipa mafanikio Brazil.


5. Kawaacha Mbali Waliokuwa Wanashindanishwa Nae

5Mbrazil huyu amekuwa kiwango cha juu sana msimu uliopita na zaidi msimu huu. Unapojaribu kumlinganisha na wachezaji wa kizazi chake kama Eden Hazard, Antoine Griezmann, Gareth Bale utofauti wa uelewa wa mchezo na kukua kwa Neymar. Anausoma mchezo vyema zaidi kuliko alivyokuwa Santos, anajua wapi anatakiwa kukimbia na mpira na wapi kwa kupasia na hazidishi manjonjo kama ilivyokuwa mwanzoni. Uhamisho wake kwenda Barcelona umemsaidia katika kukua kiuchezaji na kuboreka zaidi katika mchezaji hatari zaidi, hizi ni ishara halisi za mchezaji mwenye ubora wa kuwa bora duniani.a
Continue reading

Tuesday, December 8, 2015

Hatua ya makundi ya mechi za Klabu Bingwa barani Ulaya inamalizika leo Jumanne ya December 8 na Jumatano ya December 9 kwa mechi 16 kupigwa katika viwanja mbalimbali barani Ulaya, baada ya kupigwa michezo hii ndio tutapata picha halisi ya timu gani 16 zimefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora kati ya timu 32 zinazoshiriki michuano hiyo, licha ya kuwa kuna baadhi ya timu zimeshajithibitishia kufuzu hatua ya 16 toka mechi zilizopita ikiwemo FC Bayern Munich. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee ratiba kamili ya mechi 16 zitakazofunga hatua ya Makundi.
1
Mechi zote hizi zitachezwa Jumanne ya December 8 Saa 22:45 kwa saa za Afrika Mashariki
2
Mechi zote hizi zitachezwa Jumatano ya December 9 Saa 22:45 kwa saa za Afrika Mashariki
Continue reading

 Sir Alex: Itakuwaujinga kumfuta Mourinho
Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United,Sir Alex Ferguson ,amesema ''itakuwa ujinga'' mmiliki wa Chelsea Roman Abrahimovich kumfuta kazi Jose Mourinho
Mabingwa hao watetezi wamesalia katika nafasi ya 14 baada ya kupoteza mechi 8 kati ya 15 za kwanza msimu huu.
Duku duku zinasema kuwa kibarua cha kocha huyo mbishi huenda kikaota nyasi endapo the Blues watashindwa tena katika mechi zao 2 zijazo.
Hata hivyo kocha mwenza Ferguson amemtetea akisema hakuna haja ya kumtimua kocha huyo mwenye tajriba kuu kufuatia msimu huu mbaya.
Ferguson badala yake anapendekeza Abrahimovich avumilie kidogo upepo huu mbaya ukipita kocha Mourinho atairejesha timu hiyo katika mahala inakostahili.
''hakuna haja ya kufuta mmoja wa wakufunzi hodari kama Jose''
''Tayari amewafuta kazi watu wengi sana katika kipindi cha miaka 10 tu tangu ainunue klabu hiyo ya Stamford Bridge''
"nafkiri kufikia sasa ameshajua kuwa haifai hivyo.''
Image caption ''Sharti awe na imani, Mourinho ameshinda vikombe vikubwa kila taifa alikoenda, itakuwa ni ujinga kumfuta kazi.'' Ferguson
 

''Sharti awe na imani, Mourinho ameshinda vikombe vikubwa kila taifa alikoenda, itakuwa ni ujinga kumfuta kazi.''
'Hiyo bila shaka ni usimamizi duni.'
Mourinho alirejea Chelsea mwaka wa 2013 na akatwaa kombe la Capital One.
Taji hilo linaongezea kwa yale ya , FA mbali na mataji mawili ya ligi kuu ya Uingereza alizoshinda mwaka wa 2004 na 2007.
Alipotoka Stamford Bridge alishinda mataji mawili akiwa na Inter Milan na mawili akiwa kocha wa vigogo wa ligi ya Uhispania Real Madrid.
"Hii ndio mara ya kwanza kwake kukosa ushindi wa aina yeyote tangu awe kocha alisema Ferguson katika hadhara ya TechCrunch Disrupt London .
''bila shaka atapata suluhu ya mkwamo huu Stamford Bridge.''
Jumamosi ijayo Chelsea itachuana na vinara wa ligi hiyo Leicester, chini ya kocha wao mpya Claudio Ranieri
Leicester wana alama 17 zaidi ya Chelsea.
Continue reading

Nahodha wa Timu ya Baseball ya Kibasila Pius Peter (kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi ya mchezo huo unavyochezwa. Kushoto ni Nahodha wa Timu ya Baseball ya Tigers Mussa Mbugi.
Nahodha wa Timu ya Baseball ya Kibasila Pius Peter (wa pili kulia ) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Mashindano ya Kitaifa ya Awamu ya Tatu ya Mchezo wa Baseball yanayotarajia kuanza Ijumaa ya wiki hii jijini Dar es salaam . Wengine Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Baseball nchini Alpherio Nchimbi(kushoto) ,Nahodha wa Timu ya Baseball ya Tigers Mussa Mbugi( wa pili kushoto) na Nahodha wa Timu ya Baseball ya Giants Douglas Stanslaus.(kulia).

Na Nyakongo Manyama- MAELEZO.


MASHINDANO ya Kitaifa ya Awamu ya Tatu ya Mchezo wa Baseball yanatarajiwa kuanza Ijumaa ya wiki hii jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Baseball nchini Alpherio Nchimbi leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Amesema kuwa mashindano yatashirikisha timu tisa kutoka Tanzania bara na Visiwani na yanatarajiwa kufunguliwa na Balozi wa Japani nchini Tanzania Mhe. Masaharu Yoshida.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo , mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika shule ya Sekondari ya Azania iliyopo jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa mashindano hayo yanayojulikana kama 3rd Koshien Tanzania National Championship yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanza tarehe 11 hadi 13 mwezi huu.

Nchimbi amezitaja timu zitakazoshiriki kuwa ni Shule za Sekondari ya Azania, Kibasila , Iyunga, Sanya Juu, Londoni , na Mwanza Baseball Club, Mwanakwerekwe “C” , Tigers na Giants.




Amesema kuwa mshindano ya mwaka huu yanatarajiwa kusimamiwa na wataalamu kutoka nchini Japan wakishirikiana na wataalam kutoka nchini katika kutoa uamuzi na masuala mengine ya kiufundi.

Nchimbi amesema lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya Taifa ya umri wa chini ya miaka 21 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kushiriki mashindano yatakayofanyika Afrika kusini hapo mwezi wa pili(February ) mwakani (2016).
Kwa upande wa Nahodha wa Timu ya Giants Douglas Stanslaus ametoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kwa ajili kuona mashindano hayo na kuwatia moyo ili waweze kukuza mchezo huo nchini.
Naye Nahodha kwa timu ya Kibasila Pius Peter amewaomba vijana wengi kujitokeza kuona na kujifunza jinsi mchezo huo unavyochezwa ili hatimaye mchezo huo umeweze kuenea sehemu mbalimbali nchini kama fursa ya vijana kushirikiana na kujenga umoja.
Aidha Katibu Mkuu wa Katibu wa Chama cha Mchezo wa Baseball nchini Nchimbi amewaomba wadau mbalimbali kuthamini mchezo wa Baseball kama ilivyo michezo mingine na kujitokeza kuufadhili ili uweze kukua na kutengeneza ajira kwa vijana.
Continue reading

Monday, December 7, 2015

Mchezo wa mpira wa miguu ndiyo mchezo unaoongoza kwa kupendwa na kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni kote, vilabu vikubwa vya soka vimekuwa na mashabiki wengi katika kila pembe ya dunia na hii inatokana na kufanya vizuri kwa vilabu hivyo.
Hapa nakuletea vilabu 10 vyenye mashabiki wengi wanaovipenda vilabu vyao duniani kote.
10. Juventus –mashabiki milioni 22 duniani kote
ten 9
Mabingwa wa ligi ya Italia na finalists wa michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu wa 2014/2015 timu ya Juventus ndiyo klabu inayoshikilia nafasi ya 10 kwa kuwa na mashabiki wengi duniani.
9. Bayern Munich- mashabiki milioni 26 duniani
ten 8
Mabingwa wa Bundesliga na mabingwa wa klabu bingwa mwaka 2014 ndiyo klabu kubwa kwa upande wa Ujerumani huku ikikamatia nafasi ya tisa kwa kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni.
8. Inter Milan-mashabiki milioni 51 duniani
ten 7
Timu hiyo iliyowahi kushinda treble mwaka 2010 ikiwa chini ya kocha wa sasa wa Chelsea Jose Mourinho, haijapata tena mafanikio baada ya kuondoka kwa Mourinho lakini bado ni klabu yenye nguvu ikiwa inashikilia nafasi ya nane kwa kuwa na mashabiki wengi.
7. Liverpool-mashabiki milioni 74 duniani
ten 6
Kikosi hicho cha Anfield kinafahamika kwa kuwa na mashabiki wa kweli wanaoipenda timu yao toka moyoni  duniani kote. Liverpool bado inatazamwa kama  ndiyo klabu ambayo ilitwaa ubingwa wa Ulaya kwa style ya aina yake baada ya kutoka nyuma kwa bao 3-0 hadi kunyakua kombe hilo mbele ya AC Milan mwka 2005.
Timu hiyo wakati ikiwa chini ya kocha Brendan Rodgers ilikaribia kutwaa ubingwa wa EPL mwaka 2014 lakini ilishindwa kufanya hivyo na sasa imefikisha miaka 21 tangu itwae taji hilo kwa mara ya mwisho. Liverpool inasifika kuwa moja ya klabu ambazo zinamashabiki wanaoshangilia zaidi duniani.
6. AC Milan-mashabiki milioni 105 ulimwenguni
ten 5
Klabu ya pili kwa rekodi ya kutwaa taji la klabu bingwa Ulaya ikiwa imetwaa taji hilo mara saba. Wababe hao wa Italia wamekuwa katika wakati mgumu katika miaka ya hivi karibuni baada ya kuondoka kwa kocha Carlo Ancelotti. Mashabiki wake bado ni wengi katika kila pembe ya dunia.
5. Arsena-mashabiki milioni 125
ten 4
Wanafahamika kwa kuisifia klabu yao kwamba ndiyo klabu bora ulimwenguni, kuanzia Afrika, Asia na Amerika wanasimama na kusema watashinda taji la ligi ya mabingwa Ulaya lakini hilo halijafanikiwa hadi sasa.
Namba yao inazidi kuongezeka kila kukicha hususan katika bara la Asia na Afrika. Wanasimama katika nafasi ya tano.
4. Chelsea-mashabiki milioni 145 duniani
ten 3
Mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu England ni miongoni mwa klabu ambazo mashabiki wake wanaongezeka kwa kasi kati ya klabu 50 za Ulaya. Timu hiyo yenye makazi yake London ilianza kununua wacheaji wenye majina makubwa baada ya ujio wa tajiri wa Russia kwenye klabu hiyo Roman Abramovic.
Chelsea ilishinda kombe la klabu bingwa Ulaya mwaka 2012 kwa kuifunga Bayern Munich kwenye uwanja wao wa nyumbani. Mashabiki wa timu hiyo kwa upande wa Afrika wameendelea kuongezeka siku hadi siku.
3. Real Madrid-mashabiki milioni 195
ten 2
Licha ya kwamba kikosi cha Madrid maarufu kama Los Blancos ni klabu yenye mafanikio ulimwenguni, bado wako nyuma linapokuja suala la kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni.
2. Barcelona-mashabiki milioni 290 ulimwenguni kote
ten 1
Mabingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2015, 2011 na 2009 lakini bado hawajaweza kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa na mashabiki wengi duniani. Ni moja kati ya timu bora duniani kwa sasa wakiongozwa na nyota kama Neymar, Luis Suarez pamoja na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora duniani mara nne Lionel Messi.
1. Manchester United-mashabiki milioni 670 duniani kote
ten
Manchester United imeendelea kushika namba 1 kwa vilabu vyenye mashabiki wengi duniani. Kuanzia Marekani, Afrika, Asia, Amerika ya Kusini, na hata Ulaya, The Red Devils ndiyo klabu inayobakia kuwa kinara kwa kupendwa na kuwa na mashabiki wengi zaidi.
Hawajashinda taji lolote kwa miaka miwili sasa tangu kuondoka kwa kocha wa muda mrefu wa timu hiyo Sir. Alex Ferguson. Hiyo haijawaathiri kwa namna yeyote kimapato lakini pia hata kwa upande wa mashabiki. Imebaki kuwa klabu kubwa duniani kote hasa katika upande wa mashabiki.
Continue reading


russell

Katika moja ya kauli zake Kobe Bryant aliwahi kunukuliwa akisema anampenda Russell Westbrook anavyocheza. Sababu kubwa na katika kile kinachoitwa “Athleticism” yaani uwezo mkubwa wa kutumia kasi ya mwili, nguvu kupata matokeo.
Hii ndio silaha kubwa ya mchezaji Russell Westbrook, na hili ndilo eneo ambalo anawazidi Point guards wengine wengi. Si ajabu kumuona akawa mwepesi wa kupiga dunks, kudaka rebounds kuliko wachezaji wengine wa mbele kama power fowards.
Alfajiri ya leo hakuangusha pia, aliweza kuiongoza timu yake ya Oklahoma City Thunders dhidi ya Sacramento Kings. Russell Westbrook aliweza kumaliza mchezo huo akiwa na triple double. Alifunga pointi 19, akadaka rebound 11 hakuwa nyuma kuwasaidia wenzake, kwani alitoa pasi 10. Oklahoma City ikashinda 98-95.
Tangu timu ihamie katika jiji la Oklahoma imekuwa na matokeo ya 14-0 dhidi ya Sacramento Kings, ikumbukwe zamani ilifahamika kama Seattle Sonics. Na matokeo yao ya jumla katika uwanja wa Chesapeake Arena ni 23-4.
Durant alikuwa na moja ya michezo iliyompa shida kwani alipoteza mipira mara 10 (turnovers) lakini haikumzuia kuirejesha timu yake mchezoni. Durant alifunga pointi 4 za mwisho wakati Oklahoma ikiwa nyuma kwa pointi 95-94. Alimaliza mchezo na pointi 20 na rebound 9.
Rajon Rondo anayeongoza ligi kwa kuwa na pasi nyingi zaidi, alimaliza na pasi 10 na kufunga pointi 7. Rudy Gay aliongeza pointi 20 kwa upande wa Sacramento Kings. Bellinelli na Collison wote walimaliza na pointi 16 kwa upande wa Sacramento Kings.
Continue reading


Kipindi maalumu cha uchunguzi kinachojulikana kama BBC Panorama, kimeonesha ushahidi kwamba rais wa FIFA Sepp Blatter aliyesimamishwa kwa muda, anachunguzwa na shirika la ujajusi la Marekani, FBI.

Kuna kampuni ya masoko ya michezo inayoaminika kulipa mamilioni ya dola za Kimarekani kwa maafisa waandamizi wa FIFA katika miaka ya mwishoni mwa 1990 ili kupewa haki ya kutangaza michuano ya kombe la dunia.
Aliyekuwa ameshikia nafasi hiyo kabla ya Blatter, Joao Havelange, alikuwa ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo.
03CA7BA700000514-0-image-a-36_1449433058616
Joao Havelange
Blatter, amekana kuwa na taarifa yoyote ya sakata hilo, lakini kipindi cha Panorama kimeona barua iliyosainiwa na Joao Havelange ikisema Blatter ana taarifa kamili.

Source: BBC
Continue reading

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE