About us

Monday, December 7, 2015

RUSELL WESTBROOK AFANYA KWELI, THUNDER YAWAPIGA RADI WAFALME WA SACRAMENTO


russell

Katika moja ya kauli zake Kobe Bryant aliwahi kunukuliwa akisema anampenda Russell Westbrook anavyocheza. Sababu kubwa na katika kile kinachoitwa “Athleticism” yaani uwezo mkubwa wa kutumia kasi ya mwili, nguvu kupata matokeo.
Hii ndio silaha kubwa ya mchezaji Russell Westbrook, na hili ndilo eneo ambalo anawazidi Point guards wengine wengi. Si ajabu kumuona akawa mwepesi wa kupiga dunks, kudaka rebounds kuliko wachezaji wengine wa mbele kama power fowards.
Alfajiri ya leo hakuangusha pia, aliweza kuiongoza timu yake ya Oklahoma City Thunders dhidi ya Sacramento Kings. Russell Westbrook aliweza kumaliza mchezo huo akiwa na triple double. Alifunga pointi 19, akadaka rebound 11 hakuwa nyuma kuwasaidia wenzake, kwani alitoa pasi 10. Oklahoma City ikashinda 98-95.
Tangu timu ihamie katika jiji la Oklahoma imekuwa na matokeo ya 14-0 dhidi ya Sacramento Kings, ikumbukwe zamani ilifahamika kama Seattle Sonics. Na matokeo yao ya jumla katika uwanja wa Chesapeake Arena ni 23-4.
Durant alikuwa na moja ya michezo iliyompa shida kwani alipoteza mipira mara 10 (turnovers) lakini haikumzuia kuirejesha timu yake mchezoni. Durant alifunga pointi 4 za mwisho wakati Oklahoma ikiwa nyuma kwa pointi 95-94. Alimaliza mchezo na pointi 20 na rebound 9.
Rajon Rondo anayeongoza ligi kwa kuwa na pasi nyingi zaidi, alimaliza na pasi 10 na kufunga pointi 7. Rudy Gay aliongeza pointi 20 kwa upande wa Sacramento Kings. Bellinelli na Collison wote walimaliza na pointi 16 kwa upande wa Sacramento Kings.

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE