About us

Tuesday, January 12, 2016

Sepp Blatter: Kuwasilisha rufaa yake


Aliye kuwa raisi wa shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatterna Mwanasheria wake anatarajiwa kuwasilisha rufaa ya mteja wake ya kupinga kufungiwa miaka minane kujishughulisha na masuala ya soka.

Hata hivyo kamati ya nidhamu ya FIFA imewasilisha sababu za kuchukuliwa kwa hatua za nidhamu dhidi ya viongozi hao waandamizi wa zamani wa soka Blatter na mwenzake, Michel Platini. Mwezi Disemba aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini walifungia kwa kipindi cha miaka minane baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja kanuni na sharia za FIFA. Kwa upande wake pia mwanasheria wa Platini anasema kuwa anatarajia kukata rufaa kwa kupinga maamuzi ya FIFA.

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE