Dully Sykes amesema amefunga mlango wa kuwasaidia wasanii wachanga kwa madai aliowasaidia bado hawajamrudishia fadhila.
Mwimbaji huyo aliyeachia wimbo ‘Tuachie’ hivi karibuni akiwa na Yamoto Band, amekiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV kuwa haba tena muda wa kusaidiana bali anachohitaji ni pesa.
“Up coming artists mimi siwahitaji tena kwenye studio yangu,” alisema. “Mimi nahitaji aje alipe na bei yangu ni ile ile. Nimesaidia wengi mpaka leo wanapata pesa zao na hawanikumbuki hata kusema yule bro sisi tumetoka kwake pale tumpe hata 20,000 akanunulie nyanya. Kwahiyo mimi sihitaji kusaidia mtu. Na wasanii wangu ambao ni hao hao nafikiria nitafanya nao kazi,” alisisitiza.
Amemtaja Diamond kuwa miongoni mwa wasanii wachache waliorudisha fadhila.