About us

Friday, December 11, 2015

Sababu 5 Kwanini Neymar Atakuwa Mwanasoka Bora Wa Dunia Miezi Kadhaa Ijayo



Kwa mara ya kwanza jukwaa la Ballon D’or litapata ugeni mpya wakati mshambuliaji wa kibrazil Neymar Dos Santos atakapoungana na wafalme wawili wa tuzo hizo ambao wameitawala tuzo hiyo zaidi ya miaka 8 – Cristiano Ronaldo na Lionel Messi – itakapofika January 2016. Kama isingekuwa siasa za soka basi mbrazil huyo angeweza kushika nafasi ya pili nyuma Lionel Messi. Lakini hii ni ‘era’ mpya ya soka.
IMG_1225.JPGKatika miaka 8 iliyopita Ballon D’or imekuwa inatawalia na Messi dhidi ya Ronaldo, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda inaonekana mtu wa kupambana na Messi si Ronaldo tena ambaye umri unamtupa – anakaribia kutimiza miaka 31, Ni Neymar ambaye nyota yake inazidi kung’aa kila kukicha.
Pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana vizuri na washambuliaji wengine wa Barca, pia Neymar ameonyesha anaweza ku-control mechi kama ilivyo kwa Messi, tofauti na Ronaldo.
Wadau na wachambuzi wengi wa michezo duniani wanaamini katika kipindi kifupi kijacho Neymar atakuja kuwa mwanasoka bora zaidi duniani, mimi nikiwepo kwenye kundi hilo na hizi ndio sababu zangu.
  1. Kupafomu vyema Anapokosekana Messi 
281D9A4600000578-3060793-image-a-29_1430309883032Unapocheza pembeni ya Lionel Messi, vitu huenda kiurahisi zaidi. Wakati Messi alipoumia hivi karibuni kwa zaidi ya mwezi mmoja, wachambuzi wengi walikuwa na mashaka na uwezo wa Neymar kuziba pengo na kuisadia Barcelona kama ilivyokuwa kwa Messi. Lakini matokeo yake, Neymar akafanya vizuri zaidi katika kuisadia Barcelona kushinda kila mara na sasa wapo juu ya kilele cha msimamo wa ligi na wamefuzu raundi ya 16 bora wa UEFA Champions League. Kuziba pengo la mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kuugusa mpira sio jambo rahisi kabisa lakini kwa namna Neymar alivyohimili presha na kuifanya kazi, inaonyesha wazi dalili za world class player mwenye uwezekano wa kutwaa  Ballon d’Or hivi karibuni.
  1. Uwezo Binafsi
150606223921-neymar-champions-league-final-super-169Yes, ni kweli hivi sasa Neymar amekuwa mchezaji anayecheza kitimu zaidi kuliko ilivyokuwa zamani. Hata kuna wakati timu ikiwa inacheza vibaya, Neymar amekuwa akijitokeza na kuchukua majukumu ya timu kutumia uwezo binafsi kuiletea timu matokeo chanya. Anaweza kuchukua ‘vijiji’  kiurahisi na kuiletea madhara makubwa ngome ya timu pinzani, si rahisi kutabiri nini atafanya wakati mwingine. Ni mchezaji ambaye ni vigumu kumkaba na mbinu zake kali alizonazo miguuni na kadri anavyoendelea kucheza na kupata uzoefu, Neymar yupo njiani kuwa mwanasoka bora zaidi duniani.
3. Uwezo wa Kuwachezesha Wenzie
neymarhighs_sf6ly9x16vcg10w421p262n2m-1425743415Baadhi ya wachezaji  bora duniani wamekuwa bora kutokana na ukweli kwamba wana uwezo wa kuwachezsha wachezaji wenzao. Mchezo wa Neymar huko nyuma ulikuwa umeegemea katika uwezo wake binafsi zaidi na kuna muda alifanya iwe rahisi kwa wapinzani kuzuia dhidi ya timu yao. Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda amekuwa sehemu muhimu ya timu, Neymar ameuelewa zaidi mfumo na sasa anawachezsha mpaka wachezaji wenzie. Takwimu zinaonyesha hivi sasa anapiga sana pasi kuliko ilivyokuwa zamani, hili la kupiga pasi limeongeza kutokutabirika kwa mchezo wake na kuzidi kuwapa wakati mgumu wanaomzuia kumkaba. Hili limeleta mabadiliko makubwa katika staili ya uchezaji wa Neymar – pia limemletea mafanikio kuliko mwanzoni.
  1. Influence in the International side :
Neymar of Brazil celebrates his second goal against Turkey during their international friendly soccer match at Sukru Saracoglu stadium in Istanbul November 12, 2014. REUTERS/Murad Sezer (TURKEY  - Tags: SOCCER SPORT)Wanaompinga Neymar wana utetezi wao kwamba mchezaji huyo anafanya vizuri Barcelona kutokana na sapoti ya Messi na Suarez lakini kiwango cha Neymar kinapoangaliwa kwenye level ya timu ya taifa – ushahidi unaonyesha Neymar ndio msingi mkuu wa mashambulizi ya timu ya Selecao. Nahodha huyo wa Brazil ameitawala safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na ameiongoza kimafanikio mpaka sasa akiwa na miaka 23 tu. Bado ana safari ndefu kuendelea kuwa na kiwango kikubwa alichonacho. Ameyabeba majukumu ya unahodha vizuri sana na anaamini hivi karibuni ataipa mafanikio Brazil.


5. Kawaacha Mbali Waliokuwa Wanashindanishwa Nae

5Mbrazil huyu amekuwa kiwango cha juu sana msimu uliopita na zaidi msimu huu. Unapojaribu kumlinganisha na wachezaji wa kizazi chake kama Eden Hazard, Antoine Griezmann, Gareth Bale utofauti wa uelewa wa mchezo na kukua kwa Neymar. Anausoma mchezo vyema zaidi kuliko alivyokuwa Santos, anajua wapi anatakiwa kukimbia na mpira na wapi kwa kupasia na hazidishi manjonjo kama ilivyokuwa mwanzoni. Uhamisho wake kwenda Barcelona umemsaidia katika kukua kiuchezaji na kuboreka zaidi katika mchezaji hatari zaidi, hizi ni ishara halisi za mchezaji mwenye ubora wa kuwa bora duniani.a

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE