About us

Monday, December 7, 2015

UNAJUA TIMU YAKO INAMASHBIKI WANGAPI? HII HAPA TOP 10 YA TIMU ZENYE MASHABIKI WENGI DUNIANI

Mchezo wa mpira wa miguu ndiyo mchezo unaoongoza kwa kupendwa na kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni kote, vilabu vikubwa vya soka vimekuwa na mashabiki wengi katika kila pembe ya dunia na hii inatokana na kufanya vizuri kwa vilabu hivyo.
Hapa nakuletea vilabu 10 vyenye mashabiki wengi wanaovipenda vilabu vyao duniani kote.
10. Juventus –mashabiki milioni 22 duniani kote
ten 9
Mabingwa wa ligi ya Italia na finalists wa michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu wa 2014/2015 timu ya Juventus ndiyo klabu inayoshikilia nafasi ya 10 kwa kuwa na mashabiki wengi duniani.
9. Bayern Munich- mashabiki milioni 26 duniani
ten 8
Mabingwa wa Bundesliga na mabingwa wa klabu bingwa mwaka 2014 ndiyo klabu kubwa kwa upande wa Ujerumani huku ikikamatia nafasi ya tisa kwa kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni.
8. Inter Milan-mashabiki milioni 51 duniani
ten 7
Timu hiyo iliyowahi kushinda treble mwaka 2010 ikiwa chini ya kocha wa sasa wa Chelsea Jose Mourinho, haijapata tena mafanikio baada ya kuondoka kwa Mourinho lakini bado ni klabu yenye nguvu ikiwa inashikilia nafasi ya nane kwa kuwa na mashabiki wengi.
7. Liverpool-mashabiki milioni 74 duniani
ten 6
Kikosi hicho cha Anfield kinafahamika kwa kuwa na mashabiki wa kweli wanaoipenda timu yao toka moyoni  duniani kote. Liverpool bado inatazamwa kama  ndiyo klabu ambayo ilitwaa ubingwa wa Ulaya kwa style ya aina yake baada ya kutoka nyuma kwa bao 3-0 hadi kunyakua kombe hilo mbele ya AC Milan mwka 2005.
Timu hiyo wakati ikiwa chini ya kocha Brendan Rodgers ilikaribia kutwaa ubingwa wa EPL mwaka 2014 lakini ilishindwa kufanya hivyo na sasa imefikisha miaka 21 tangu itwae taji hilo kwa mara ya mwisho. Liverpool inasifika kuwa moja ya klabu ambazo zinamashabiki wanaoshangilia zaidi duniani.
6. AC Milan-mashabiki milioni 105 ulimwenguni
ten 5
Klabu ya pili kwa rekodi ya kutwaa taji la klabu bingwa Ulaya ikiwa imetwaa taji hilo mara saba. Wababe hao wa Italia wamekuwa katika wakati mgumu katika miaka ya hivi karibuni baada ya kuondoka kwa kocha Carlo Ancelotti. Mashabiki wake bado ni wengi katika kila pembe ya dunia.
5. Arsena-mashabiki milioni 125
ten 4
Wanafahamika kwa kuisifia klabu yao kwamba ndiyo klabu bora ulimwenguni, kuanzia Afrika, Asia na Amerika wanasimama na kusema watashinda taji la ligi ya mabingwa Ulaya lakini hilo halijafanikiwa hadi sasa.
Namba yao inazidi kuongezeka kila kukicha hususan katika bara la Asia na Afrika. Wanasimama katika nafasi ya tano.
4. Chelsea-mashabiki milioni 145 duniani
ten 3
Mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu England ni miongoni mwa klabu ambazo mashabiki wake wanaongezeka kwa kasi kati ya klabu 50 za Ulaya. Timu hiyo yenye makazi yake London ilianza kununua wacheaji wenye majina makubwa baada ya ujio wa tajiri wa Russia kwenye klabu hiyo Roman Abramovic.
Chelsea ilishinda kombe la klabu bingwa Ulaya mwaka 2012 kwa kuifunga Bayern Munich kwenye uwanja wao wa nyumbani. Mashabiki wa timu hiyo kwa upande wa Afrika wameendelea kuongezeka siku hadi siku.
3. Real Madrid-mashabiki milioni 195
ten 2
Licha ya kwamba kikosi cha Madrid maarufu kama Los Blancos ni klabu yenye mafanikio ulimwenguni, bado wako nyuma linapokuja suala la kuwa na mashabiki wengi ulimwenguni.
2. Barcelona-mashabiki milioni 290 ulimwenguni kote
ten 1
Mabingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2015, 2011 na 2009 lakini bado hawajaweza kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa na mashabiki wengi duniani. Ni moja kati ya timu bora duniani kwa sasa wakiongozwa na nyota kama Neymar, Luis Suarez pamoja na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora duniani mara nne Lionel Messi.
1. Manchester United-mashabiki milioni 670 duniani kote
ten
Manchester United imeendelea kushika namba 1 kwa vilabu vyenye mashabiki wengi duniani. Kuanzia Marekani, Afrika, Asia, Amerika ya Kusini, na hata Ulaya, The Red Devils ndiyo klabu inayobakia kuwa kinara kwa kupendwa na kuwa na mashabiki wengi zaidi.
Hawajashinda taji lolote kwa miaka miwili sasa tangu kuondoka kwa kocha wa muda mrefu wa timu hiyo Sir. Alex Ferguson. Hiyo haijawaathiri kwa namna yeyote kimapato lakini pia hata kwa upande wa mashabiki. Imebaki kuwa klabu kubwa duniani kote hasa katika upande wa mashabiki.

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE