About us

Friday, December 11, 2015

Kayumba wa BSS Kuelekea South Africa Kushoot Video yake mpya na Director Mkubwa nchini Humo....





Mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS) 2015, Kayumba Juma anasafiri usiku wa Ijumaa hii kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya video ya wimbo wake mpya.
Muimbaji huyo ambaye alijinyakulia kitita cha shilingi milioni 60 baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na ushindani mkubwa, atasafiri akiwa pamoja na timu ya BSS ikiongozwa na mkurugenzi wake Madam Rita.
Akizungumza na Bongo5 leo mmoja kati ya viongozi wa msanii huyo, Said Fella, amesema kila kitu kinaenda sawa katika maandalizi ya ujio wa msanii huyo.
“Kayumba yupo sawa na usiku wa leo akiwa na timu ya BSS wanaelekea South Africa kufanya video na director aliyefanya video ya Shaa. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula. Pia tarehe 16 mwezi huu atakuwa pale Dar Live kwa ajili ya show akiwa na Yamoto Band.”

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE