NEW YORK,Marekani
Mgombea mtarajiwa wa uraisi kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump ametaka Waislamu kuzuiwa kuingia nchini Marekani kwa muda.
Trump anasema utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonesha kuwa waislamu wengi wamepandikiza chuki juu ya Marekani na sasa mpaka uongozi ubaini sababu za kuwepo kwa chuki hiyo, watu wanahitaji kujilindwa.
Ikulu ya Marekeni imesema tamko la Trump linaenda kinyume na maadili ya taifa la Marekani na maslahi ya usalama wa taifa.
Tamko hilo la Donald Trump limekuja siku chache baada ya watu kumi na nne kuuwawa katika shambulio la risasi zilizopigwa katika mkusanyiko wa watu na wanandoa ambao ni Waislamu.
Shirika la kijasusi la Marekani FBI limesemaSyed Farook na Tashfeen Malik walipandikizwa itikadi kali lakini hawajui na nani na ni kwa namna gani.
FBI walioko California,wameivamia nyumba inayoshukiwa kuhusika katika shambulio hilo na kusema imepata mabomba kumi na tisa ambayo yangeweza kutumika kutengenezea mabomu katika nyumba yao iliyoko Redlands huko California.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema nyumba hiyo ni ya rafiki ambaye anaaminika kuwa alifanya manunuzi ya bunduki zilizotumika katika shambulio