About us

Tuesday, December 8, 2015

KUMBE NAIBU SPIKA WA BUNGE DKT TULIA ALIKUWA MJUMBE WA BODI YA BANDARI, ALIHUSIKA NA UPOTEVU?

“WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amefuta uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA) kuanzia jana na kuteua wajumbe wengine wapya nane wanaounda bodi hiyo.


Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Kifungu Namba 6 Kifungu Kidogo cha 2 (b) cha Sheria ya Bandari Namba 17 ya mwaka 2004, kinachompa mamlaka ya kuvunja na kuteua wajumbe wa bodi.

Sitta alitangaza uteuzi huo jijini Tanga jana wakati wa ziara ya kikazi katika Bandari ya Tanga na kisha kuzungumza na wafanyakazi katika Uwanja wa Baraka bandarini hapo.

Alisisitiza kuwa mabadiliko hayo, yametokana na vitendo vya uonevu alivyokuta vikiendelea kufanywa ndani ya TPA.

Wajumbe wapya walioteuliwa ni pamoja na Mhadhiri wa Chuo cha Sheria Tanzania, Dk Tulia Akson, Mhandisi wa Ujenzi, Norplan Consultants, Musa Ally Nyamsingwa, Mtaalamu wa Manunuzi na Mjumbe wa Bodi ya Posta, Donata Mugassa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa EWURA, Haruna Masebu.

Wengine ni Mhandisi wa Elektroniki wa Bodi ya Wahandisi Tanzania, Gema Modu, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dk Francis Michael, Mkurugenzi wa Mipango NSSF, Crescentius Magori na aliyekuwa Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Flavian Kinunda.

“Uteuzi huu unatengua uteuzi wa wajumbe wa sasa wa bodi hiyo kuanzia leo Juni 2, mwaka huu na lengo la uteuzi wa wajumbe hawa ni kuleta tija na ufanisi wa utendaji kazi ndani ya wa Mamlaka”, alisema.

Uteuzi huo umefuta ule wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, uliofanywa Novemba 6, 2012 na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe uliofanywa kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Bandari na Kifungu 1(2(i)) cha jedwali la kwanza la Sheri ya Bandari ya mwaka 2004.

Waliofutiwa ujumbe wa Bodi ni Dk Jabir Kuwe Bakari, John Ulanga, Caroline Temu, Jaffer Machano, Dk Hildebrand Shayo, Said Salum Sauko, Mhandisi Julius Mamiro na Asha Nasoro.”

MIEZI 6 BAADA YA UTEUZI

Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano Dkt.John Pombe Magufuli katika kasi yake ya kutumbua majipu hatimaye,amevunja bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa bandari Bw.Awadhi Massawe (Pichani), Mwenyekiti wa bodi ya bandari pamoja maofisa 8 wa bandari .Ameagiza wote wawekwe chini ya ulinzi kwa ajili ya uchunguzi Kufuatia kuibuka kwa upotevu wa makontena zaidi 2000 yaliyosababisha serikali kupoteza mabilioni ya fedha.

Rais  pia  amemsimamisha  kazi katibu mkuu wizara ya uchukuzi Bw.Shabani Mwinjaka.

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE