Hapatoshi! Desemba 19, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar, Yamoto Band pamoja na msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Zanzibar, Baby J wanatarajia kumtambulisha kwa mara ya kwanza mshindi wa Bongo Star Search (BSS 2015), Kayumba Juma.

“Mashabiki watarajie kupata sapraizi kibao kutoka kwa Yamoto ikiwa ni pamoja na kutambulisha wimbo wao mpya wa Imo baada ya kubamba na Cheza kwa Madoido sambamba na utambulishio wa Kayumba, yote hayo yatapatikana kwa kiingilio cha shilingi 10,000,” alisema Mudy K.