Kipindi maalumu cha uchunguzi kinachojulikana kama BBC Panorama, kimeonesha ushahidi kwamba rais wa FIFA Sepp Blatter aliyesimamishwa kwa muda, anachunguzwa na shirika la ujajusi la Marekani, FBI.
Kuna kampuni ya masoko ya michezo inayoaminika kulipa mamilioni ya dola za Kimarekani kwa maafisa waandamizi wa FIFA katika miaka ya mwishoni mwa 1990 ili kupewa haki ya kutangaza michuano ya kombe la dunia.
Aliyekuwa ameshikia nafasi hiyo kabla ya Blatter, Joao Havelange, alikuwa ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo.
Joao Havelange
Blatter, amekana kuwa na taarifa yoyote ya sakata hilo, lakini kipindi cha Panorama kimeona barua iliyosainiwa na Joao Havelange ikisema Blatter ana taarifa kamili.
Source: BBC