About us

Friday, December 11, 2015

News-Sacked
Kocha Louis Van Gaal wa Manchester United anaweza kutimka klabuni hapo mwisho wa msimu huu pamoja na kuwa bado ana mkataba hadi msimu ujao. Taarifa zilizoandikwa na magazeti mbalimbali nchini England zinasema hali sio shwari sana kwa future ya kocha Louis Van Gaal ambaye sasa presha ni kubwa sana kutokana na kutolewa kwa Manchester United klabu bingwa Ulaya sanjari na mwendo wa kobe katika ligi kuu soka nchini England.
Swali kubwa ni nani atakae rithi mikoba ya kocha huyu endapo ataondoka klabuni hapo? Alipoteuliwa kwa mara ya kwanza kuwa msaidizi mwaka 2013 mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Ryan Giggs, taa ya kijani ilianza kuwaka kwa mkongwe huyo aliyecheza kwa mafanikio sana chini ya kocha Sir Alex Ferguson.
Habari zinasema kuwa, Ryan Giggs ndiye chaguo la mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo Ed Woodward na kwamba ndiye atakaye kuwa mrithi wa Van Gaal endapo tu mholanzi huyo ataondoka Old Trafford.
Ryan Giggs amekaa na kocha Sir Alex Ferguson huku akishuhudia utawala wa Manchester United barani Ulaya na ligi za nyumbani lakini sasa amekua akiumia hali akiwa msaidizi tangu 2013. Kimya chake kinaweza kuwa cha kisiasa kuwatega United kuhusiana na kupewa nafasi ya ukocha mkuu baada ya Louis Van Gaal.
Lakini kocha wa Bayern Munich Pep Guadiola anaweza kuwa mrithi wa Van Gaal endapo tu Manchester United itaamua kutafuta mwalimu kutoka nje ya Uingereza. Tayari kuna taarifa za chinichini kuhusu nia ya Pep Guadiola kuwa na mahaba na United, huku hadi sasa akiwa hajasema chochote kuhusu mkataba wake.
Continue reading



Kwa mara ya kwanza jukwaa la Ballon D’or litapata ugeni mpya wakati mshambuliaji wa kibrazil Neymar Dos Santos atakapoungana na wafalme wawili wa tuzo hizo ambao wameitawala tuzo hiyo zaidi ya miaka 8 – Cristiano Ronaldo na Lionel Messi – itakapofika January 2016. Kama isingekuwa siasa za soka basi mbrazil huyo angeweza kushika nafasi ya pili nyuma Lionel Messi. Lakini hii ni ‘era’ mpya ya soka.
IMG_1225.JPGKatika miaka 8 iliyopita Ballon D’or imekuwa inatawalia na Messi dhidi ya Ronaldo, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda inaonekana mtu wa kupambana na Messi si Ronaldo tena ambaye umri unamtupa – anakaribia kutimiza miaka 31, Ni Neymar ambaye nyota yake inazidi kung’aa kila kukicha.
Pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana vizuri na washambuliaji wengine wa Barca, pia Neymar ameonyesha anaweza ku-control mechi kama ilivyo kwa Messi, tofauti na Ronaldo.
Wadau na wachambuzi wengi wa michezo duniani wanaamini katika kipindi kifupi kijacho Neymar atakuja kuwa mwanasoka bora zaidi duniani, mimi nikiwepo kwenye kundi hilo na hizi ndio sababu zangu.
  1. Kupafomu vyema Anapokosekana Messi 
281D9A4600000578-3060793-image-a-29_1430309883032Unapocheza pembeni ya Lionel Messi, vitu huenda kiurahisi zaidi. Wakati Messi alipoumia hivi karibuni kwa zaidi ya mwezi mmoja, wachambuzi wengi walikuwa na mashaka na uwezo wa Neymar kuziba pengo na kuisadia Barcelona kama ilivyokuwa kwa Messi. Lakini matokeo yake, Neymar akafanya vizuri zaidi katika kuisadia Barcelona kushinda kila mara na sasa wapo juu ya kilele cha msimamo wa ligi na wamefuzu raundi ya 16 bora wa UEFA Champions League. Kuziba pengo la mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kuugusa mpira sio jambo rahisi kabisa lakini kwa namna Neymar alivyohimili presha na kuifanya kazi, inaonyesha wazi dalili za world class player mwenye uwezekano wa kutwaa  Ballon d’Or hivi karibuni.
  1. Uwezo Binafsi
150606223921-neymar-champions-league-final-super-169Yes, ni kweli hivi sasa Neymar amekuwa mchezaji anayecheza kitimu zaidi kuliko ilivyokuwa zamani. Hata kuna wakati timu ikiwa inacheza vibaya, Neymar amekuwa akijitokeza na kuchukua majukumu ya timu kutumia uwezo binafsi kuiletea timu matokeo chanya. Anaweza kuchukua ‘vijiji’  kiurahisi na kuiletea madhara makubwa ngome ya timu pinzani, si rahisi kutabiri nini atafanya wakati mwingine. Ni mchezaji ambaye ni vigumu kumkaba na mbinu zake kali alizonazo miguuni na kadri anavyoendelea kucheza na kupata uzoefu, Neymar yupo njiani kuwa mwanasoka bora zaidi duniani.
3. Uwezo wa Kuwachezesha Wenzie
neymarhighs_sf6ly9x16vcg10w421p262n2m-1425743415Baadhi ya wachezaji  bora duniani wamekuwa bora kutokana na ukweli kwamba wana uwezo wa kuwachezsha wachezaji wenzao. Mchezo wa Neymar huko nyuma ulikuwa umeegemea katika uwezo wake binafsi zaidi na kuna muda alifanya iwe rahisi kwa wapinzani kuzuia dhidi ya timu yao. Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda amekuwa sehemu muhimu ya timu, Neymar ameuelewa zaidi mfumo na sasa anawachezsha mpaka wachezaji wenzie. Takwimu zinaonyesha hivi sasa anapiga sana pasi kuliko ilivyokuwa zamani, hili la kupiga pasi limeongeza kutokutabirika kwa mchezo wake na kuzidi kuwapa wakati mgumu wanaomzuia kumkaba. Hili limeleta mabadiliko makubwa katika staili ya uchezaji wa Neymar – pia limemletea mafanikio kuliko mwanzoni.
  1. Influence in the International side :
Neymar of Brazil celebrates his second goal against Turkey during their international friendly soccer match at Sukru Saracoglu stadium in Istanbul November 12, 2014. REUTERS/Murad Sezer (TURKEY  - Tags: SOCCER SPORT)Wanaompinga Neymar wana utetezi wao kwamba mchezaji huyo anafanya vizuri Barcelona kutokana na sapoti ya Messi na Suarez lakini kiwango cha Neymar kinapoangaliwa kwenye level ya timu ya taifa – ushahidi unaonyesha Neymar ndio msingi mkuu wa mashambulizi ya timu ya Selecao. Nahodha huyo wa Brazil ameitawala safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na ameiongoza kimafanikio mpaka sasa akiwa na miaka 23 tu. Bado ana safari ndefu kuendelea kuwa na kiwango kikubwa alichonacho. Ameyabeba majukumu ya unahodha vizuri sana na anaamini hivi karibuni ataipa mafanikio Brazil.


5. Kawaacha Mbali Waliokuwa Wanashindanishwa Nae

5Mbrazil huyu amekuwa kiwango cha juu sana msimu uliopita na zaidi msimu huu. Unapojaribu kumlinganisha na wachezaji wa kizazi chake kama Eden Hazard, Antoine Griezmann, Gareth Bale utofauti wa uelewa wa mchezo na kukua kwa Neymar. Anausoma mchezo vyema zaidi kuliko alivyokuwa Santos, anajua wapi anatakiwa kukimbia na mpira na wapi kwa kupasia na hazidishi manjonjo kama ilivyokuwa mwanzoni. Uhamisho wake kwenda Barcelona umemsaidia katika kukua kiuchezaji na kuboreka zaidi katika mchezaji hatari zaidi, hizi ni ishara halisi za mchezaji mwenye ubora wa kuwa bora duniani.a
Continue reading

Dully

Dully Sykes amesema amefunga mlango wa kuwasaidia wasanii wachanga kwa madai aliowasaidia bado hawajamrudishia fadhila.

Mwimbaji huyo aliyeachia wimbo ‘Tuachie’ hivi karibuni akiwa na Yamoto Band, amekiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV kuwa haba tena muda wa kusaidiana bali anachohitaji ni pesa.
“Up coming artists mimi siwahitaji tena kwenye studio yangu,” alisema. “Mimi nahitaji aje alipe na bei yangu ni ile ile. Nimesaidia wengi mpaka leo wanapata pesa zao na hawanikumbuki hata kusema yule bro sisi tumetoka kwake pale tumpe hata 20,000 akanunulie nyanya. Kwahiyo mimi sihitaji kusaidia mtu. Na wasanii wangu ambao ni hao hao nafikiria nitafanya nao kazi,” alisisitiza.
Amemtaja Diamond kuwa miongoni mwa wasanii wachache waliorudisha fadhila.
Continue reading





Mshindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS) 2015, Kayumba Juma anasafiri usiku wa Ijumaa hii kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya video ya wimbo wake mpya.
Muimbaji huyo ambaye alijinyakulia kitita cha shilingi milioni 60 baada ya kuibuka mshindi katika kinyang’anyiro hicho kilichokuwa na ushindani mkubwa, atasafiri akiwa pamoja na timu ya BSS ikiongozwa na mkurugenzi wake Madam Rita.
Akizungumza na Bongo5 leo mmoja kati ya viongozi wa msanii huyo, Said Fella, amesema kila kitu kinaenda sawa katika maandalizi ya ujio wa msanii huyo.
“Kayumba yupo sawa na usiku wa leo akiwa na timu ya BSS wanaelekea South Africa kufanya video na director aliyefanya video ya Shaa. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula. Pia tarehe 16 mwezi huu atakuwa pale Dar Live kwa ajili ya show akiwa na Yamoto Band.”
Continue reading



Staa wa muziki wa HipHop kutoka Marekani, Nicki Minaj maarufu pia kama The Rap Queen anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani.
minaj6
Baada ya kuchaguliwa kwenye vipengele vitatu vya The 58th Grammy Nominations, staa huyo kutoka lebo ya Cash Money Records alichukuwa time na kufanya interview na jarida kubwa la burudani Marekani, Billboard Magazine na kugusia vitu vingi ikiwemo maisha yake na Meek Mill, Siasa, Muziki, ushauri wa kimaisha  na vitu vingine kibao.
minaj4
Nicki Minaj: Billboards The No.1s Photo Shoot Cover.
Hivi ni vichache nilivyofanikiwa kuvinasa kutoka kwenye interview hiyo na Billboard Magazine:
Support anayotoa kwa Hillary Clinton: “Ninamsupport Hillary kama mwanamke. Kama nimeshawishika anafaa kuwa Rais wa awamu ijayo? Bado napenda niwe na mawazo huru kuhusu kila mgombea. Bila ubishi naelewa struggle anayoipata kama mwanamke. Pia bila ubishi naelewa nafasi anayowekwa kama mwanamke akiingia sehemu ambayo imejaa wanaume zaidi- kuna wakati naamini hata yeye anaogopa, lakini pia naamini anatumia uoga huo kama silaha yake ya ushujaa. Kwa sababu kama mwanamke nimekuwa nikifanya hivyo kila mara. Kwahiyo kwa hilo ninamkubali sana“.
minaj1
Nicki Minaj: Billboard The No.1s Issue Photo Shoot.
Kuhusu mgombea mwenza wa Hillary Clinton, Donald Trump: “Kuna hoja ameziongelea ambazo naamini kama asingetumia approach ya kitoto kuzifikisha mbele ya umma zilikuwa ni nzuri kwa namna yake. Lakini kwa upande wa burudani- huyu jamaa anachekesha sana. Natamani kama wangetengeneza movie ya yeye akiwa kwenye safari ya Urais. Hiyo ingekuwa reality show kubwa balaa.“
minaj3
Kuhamia Los Angeles na Meek Mill: “Napapenda [Los Angeles]. Nilipokuwa nahamia nilizungumza na Beyonce, kwasababu na yeye amehamia huku hivi karibuni pia. Beyonce alisema kile nilichokisema mimi mara ya kwanza nahamia huku, ambacho ni kila mmoja amekuwa mwenye furaha zaidi. Alikuwa ananiambia vitu vidogo ambavyo pengine ningeviona kama mzigo kumbe sio mzigo hata [kwa huku]. Pia aliniambia haichoshi kuamka asubuhi sana na kumpeleka Blue [mwanae] shule, kwasababu mazingira ni mazuri [na ndicho nachokiona pia].“
minaj8
Pete aliyopewa Nicki Minaj na mpenzi wake Meek Mill hivi karibuni.
Je, vipi kuhusu pete aliyovalishwa na Meek Mill: “Mimi na yeye hatupo-engaged. Lakini alisema angependa kunipa pete tatu kabla hajanioa. Birthday yangu inakuja, kwahiyo achangamke kunipa pete nyingine, kwasababu alishanipa moja [ya kwanza ilikuwa mwaka jana] kwenye birthday yangu iliyopita.“
minaj2
Jay Z, Beyonce, Nicki Minaj & Meek Mill.
Ushauri kutoka kwa Beyonce na Jay-Z: “Tuliongea nao, Jay Z na Beyonce [kuhusu ndoa]. Baada ya show yetu [Brooklyn] ya Barclays Center [ mwezi October], tulipata dinner pamoja. Walitupa ushauri mzuri sana. Nawapenda sana. Yalikuwa maongezi mazuri sana na watu tunaowapenda na kutazama kile wanachokifanya kama couple. Ile couple [Jay Z na Beyonce]  ipo mahiri sana!“
minaj5
Kama atarudi kufanya mixtape zozote: “Kabisa. Lazima niachie mixtape soon. Nataka niguse beats tofauti ambazo sikuzigusa hapo awali. Ningeweza kutoa single zenye beats nzito mwaka jana, lakini kwangu jambo la msingi ni kuonyesha mfano kwa marappers wengine wa kike. Kwenye game nipo juu sasa hivi na ni muhimu kuweka mfano… ni muhimu kwa wewe kuwa mkubwa kuliko muziki wako. Nina mashabiki amabao wameshajitoa kuwa na mimi maisha yangu yote kwasababu wanajua nilipoanzia. Mashabiki wanajua msoto wangu, jinsi nilivyokuwa na njaa, kwamba nilikuwa siridhiki na mafanikio madogo tu, sikukata tamaa, nilikuwa kwenye ngoma ya kila mtu na nilikuwa kikazi zaidi… mashabiki wanajua kwa hiyo ni lazima nifanye kazi kuonyesha mfano.“
Continue reading

 
Najua nina watu ambao wanapenda kwenda Cinema kila weekend, sasa kama upo Dar es salaam na Arusha movie zinazoonyeshwa kwenye big screen weekend hii na Trailers zake nimekuwekea hapa.
CINEMAAAAAAAA

Continue reading

Thursday, December 10, 2015

mg5
Kuelekea ukumbi wa mikutano Ikulu.
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ametangaza baraza la mawaziri December 10 2015 ambapo hata hivyo hajamaliza kutaja mawaziri wengine akisema anaangalia ni nani wa kumuweka kwenye hizo wizara zilizobaki
mg8
mg3
mg2
mg4
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Rais Magufuli na Waziri mkuu Majaliwa
mg7
Picha ya pamoja na Waandishi wa habari
mg6
Rais Magufuli, Katibu mkuu kiongozi Sefue, Waziri mkuu Majaliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Picha zote ni kutoka Ikulu.
Continue reading

Baada ya kupita kwenye headlines za MTV BASE, December 10 2015 ndio msanii wa bongofleva Jux ameiachia hii video mpya ya ‘one more night’ bonyeza play kuitazama hapa chini kisha achia comment yako Jux akipita baadae ajue watu wake wanasemaje.

Continue reading


Ni headlines za Serikali ya Rais Magufuli kwenye kazi na kasi yake kila kona… unajua sio kila kiongozi anayeshika nafasi ya juu kwenye nchi yoyote anaweza kujadiliwa kwenye vyombo vikubwa, lakini Rais Magufuli kaipata hiyo nafasi kutokana na maamuzi yake toka siku ya kwanza kaapishwa na kuingia Ikulu.
Prof. Patrick Otieno Lumumba ni mmoja ya wachambuzi wakubwa sana kwenye masuala ya siasa Afrika, amepewa airtime ya dakika tatu kuujadili ule usafi uliopigwa jana Tanzania huku Rais Magufuli, Mama Samia Suluhu na Waziri Mkuu Majaliwawakiongoza jahazi… huyu hapa kwenye dakika 3  za BBC Swahili.



Continue reading

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE