Mtaani watu wanasema wimbo wa Joh Makini ‘Don’t Bother’ huenda ukawa sababu ya kwanini ‘Baba Swalehe’ ya Nick wa Pili haikupata attention ilivyotarajiwa.
Wengine wanaamini kuwa wimbo huo alioshirikishwa pia rapper wa Afrika Kusini, AKA, huenda ukawa ni mchawi kwa wimbo huo wa Nick wa Pili.
Lakini watu wanasahau kuwa wawili hawa ni ndugu na chochote kinachotokea kati yao ni faida kwa brand yao ya Weusi. Maana yake ni kuwa ni mafanikio ya Joh Makini ni mafanikio ya Nick wa Pili na G-Nako pia.
Akiongea na Clouds FM hivi karibuni, Nick alisema Don’t Bother haijaiathiri Baba Swalehe kwa namna yoyote ile na mwisho wa siku ‘they are family.’ Jiulize pia kwanini Nick alimtumia G-Nako kwenye kava kubeba uhusika wa Baba Swalehe