About us

Tuesday, December 8, 2015

Hanscana aeleza alichojifunza SA kuhusu video nyingi za wabongo kutochezwa MTV na Trace


Baadhi ya wasanii wa Bongo ambao wamewahi kutuma video zao kwenye vituo vya MTV na Trace huwa wanaamini kuwa vituo hivyo vinaupendeleo, kutokana na kucheza video za wasanii wachache tu wa Tanzania licha ya wengi kujaribu kutuma kazi zao.

Director wa video nchini Hanscana alienda Afrika Kusini hivi karibuni, na miongoni mwa mambo aliyoyafanya huko ni pamoja na kujifunza jinsi ya kufanya kazi kwa kiwango cha kimataifa, na kutafuta ‘password’ za mageti ya kupeleka kazi zake kwenye channel za kimataifa.
Hanscana ambaye alitembelea ofisi za Trace na MTV Base za Afrika Kusini na kuonana na wahusika wa ‘jikoni’, ameshare na wengine kile alichojifunza huko, hasa kuhusu vitu vinavyosababisha video nyingi za wasanii wa Tanzania zishindwe kuchezwa.
“Kule cha kwanza ambacho kinakwamisha ni fanbase ya msanii ndio inakwamisha sana sana sana” amesema Hanscana kupitia 255 ya XXL.
“Ukiongelea kitu kama MTV Base au Trace ukiongelea kwanza Trace Nigeria hiyo ni sawa sawa umeongelea Clouds Tanzania, lazima msanii wa Tanzania apewe 60 nje ya Tanzania apewe 40, sasa katika ile 40 inakuwa ina ushindani mkubwa sana unajua asilimia 40 jnsi gani ilivyokuwa ndogo halafu nchi zilizokuwa nyingi. Kwa hiyo hadi ufike pale fanbase yako iwe vizuri yaani msanii mwenyewe fanbase yako iwe vizuri.” alifafanua.
Hanscana amewashauri wasanii wa Bongo kujitangaza na kuweka mizizi nyumbani kwanza, kuongeza fanbase kwenye mitandao ya kijamii na kuhakikisha anakuwa na views za kutosha Youtube kabla ya kufikiria kuanza kutafuta nafasi ya kuchezwa kwenye channel za kimataifa.

“Ndio maana unaweza ukaona kuna baadhi ya ngoma za wabongo zilichezwa MTV labda siku mbili siku tatu baada ya hapo hujawahi kuziona tena, wale wanaangalia je hiyo ngoma huko Tanzania inapigwa?” alisema Hans.

ADS

ADS

ADVATISE HERE

ADVATISE HERE